-
Je, taarifa zangu binafsi kwenye KKKT Digital zina salama?
Ndiyo. KKKT Digital inatumia viwango vya kimataifa vya encryption na sera madhubuti za faragha ili kulinda taarifa zako binafsi.
-
Je, kuna malipo yoyote ya kutumia KKKT Digital?
KKKT Digital inatoa huduma kulingana na vipengele mbalimbali. Kila kipengele kina thamani tofauti kulingana na huduma zinazopatikana kama vile idadi ya jumbe zinazosambazwa, elimu mbalimbali za kimaisha kama ujasiriamali, teknolojia na mengineyo.
-
Ni kwa namna gani mfumo huu unawezesha mawasiliano ndani ya kanisa?
KKKT Digital inawezesha mawasiliano kwa kufikia wanachama kwa wengi kwa wakati mmoja na kwa urahisi kupitia njia za mawasiliano kama SMS, WhatsApp, na Barua pepe. Hii inahakikisha wanachama wanapata taarifa muhimu haraka na kwa urahisi, huku kanisa likiimarisha uhusiano na mshikamano wa kijumuiya.
-
Nani anastahili kujiunga na kutumia mfumo huu?
KKKT Digital imeundwa kwa ajili ya waumini wote wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Jukwaa hili linahusisha waumini wa dayosisi zote likiwa daraja la kuwezesha mawasiliano kidijitali ndani ya kanisa la kilutheri Tanzania.
-
Je, ni hatua gani mahususi zitakazochukuliwa ili kuhakikisha kwamba ujumbe unawafikia walengwa husika?
KKKT Digital itahakikisha ujumbe sahihi unawafikia walengwa kwa kutumia uchambuzi wa taarifa na kugawa kwa makundi kulingana na umri, parokia, au maslahi ya kiroho. Mfumo pia unarahisisha urekebishaji wa ujumbe ili kufikia makundi maalum kama vijana, wazee au familia. Hivyo, kila muumini anapata taarifa, maombi, taarifa za matukio na mahubiri yanayomhusisha moja kwa moja.